SOMOLANNE;- MWANAMKE ANA JUKUMU LA KUURUDISHA UTAWALA WA MUNGU DUNIANI.


Episode Artwork
1.0x
0% played 00:00 00:00
Mar 20 2021 21 mins  
SOMOLANNE:- MWANAMKE ANA JUKUMU LA KUURUDISHA UTAWALA WA MUNGU DUNIANI. MWANZO 3: 14 Bwana Mungu akamwambia nyoka, Kwa sababu umeyafanya hayo, umelaaniwa wewe kuliko wanyama wote, na kuliko hayawani wote walioko mwituni; kwa tumbo utakwenda, na mavumbi utakula siku zote za maisha yako; 15 nami nitaweka uadui kati yako na huyo mwanamke, na kati ya uzao wako na uzao wake; huo utakuponda kichwa, na wewe utamponda kisigino. Msitari wa 15; Mungu ameweka uadui kati ya mwanamke na shetani. Lakini kwa sababu ya roho ya uasi inaitawala dunia bado mwanamke anapenda kulekule kwa shetani kutafuta msaada kwa ajili ya mume wake na watoto na hata familia ya babake na mamake!! Kwa hiyo shetani amekua akitegemewa na wanawake kuleta suluhisho la maisha, wakati huyohuyo shetani ndiye alileta balaa hili zito duniani la kutugombanisha na kututenganisha na Muumba wetu!!?? Hii inawezekana vipi?? Ili mimi na wewe tuweze kuaminiwa na Mungu kurudisha mahusiano ya mwanadamu na Mungu tuliyoyapoteza ni lazima kwanza MWANAKME UTAKASIKE! Uwe na moyo safi. Kama tulivyoanza kwenye somo la kwanza. MATHAYO 5: 8 Heri wenye moyo safi; Maana hao watamwona Mungu. Ili uwe na moyo safi huna budi kumpa Mungu nafasi ausafishe na autakase moyo wako. Sababu kama moyo wako si safi 100%, bado shetani anakua ana vitu vyake moyoni mwako, na anaweza kukurudisha tena matopeni na ukatumia vibaya utawala wa dunia uliopewa na Mungu. "Maana watamuona Mungu" Maana yake ni kufunguliwa macho yako ya ndani ufahamu wako kutiwa Nuru kama tunayojifunza hapa. MWANZO 1: 3 Mungu akasema, Iwe nuru; ikawa nuru. Cha kwanza kama hujaokoka ama hujaamua 100% kumpa Bwana Yesu maisha yako ili alete Nuru kwenye moyo wako. Hili ni jambo la kwanza kabisa Mungu alilifanya katika uumbaji ni kuumba Nuru. Na ili Mungu afanye Kazi zake hapa duniani kupitia mwanamke ni lazima awe ametakasika ndipo Mungu anakua uhakika kuwa hatazuiliwa na hatachafuliwa Kazi yake. Mimi na wewe kama wanawake, wasichana, mke, shangazi, mama mdogo, wifi, shemeji, mama mkwe, nk matendo ama matunda yangu yanaleta Uhai na Uzima popote nilipo?? Wagalatia 5: 22 Lakini tunda la Roho ni upendo, furaha, amani, uvumilivu, utu wema, fadhili, uaminifu, 23 upole, kiasi; juu ya mambo kama hayo hakuna sheria. MWANZO 3: 6 Mwanamke alipoona ya kuwa ule mti wafaa kwa chakula, wapendeza macho, nao ni mti wa kutamanika kwa maarifa, basi alitwaa katika matunda yake akala, akampa na mumewe, naye akala. Ni vitu vingapi kama mwanamke umemlisha mumeo na ikawa balaa?! Inaweza ikawa; neno, chakula, tendo, nk. Unaweza kuwa kabisa umevitoa kwa wachawi (waganga) au watumishi wa Mungu wa uwongo! MATHAYO 7: 15 Jihadharini na manabii wa uongo, watu wanaowajia wamevaa mavazi ya kondoo, walakini kwa ndani ni mbwa-mwitu wakali. 16 Mtawatambua kwa matunda yao. Je! Watu huchuma zabibu katika miiba, au tini katika mibaruti? 17 Vivyo hivyo kila mti mwema huzaa matunda mazuri; na mti mwovu huzaa matunda mabaya. 18 Mti mwema hauwezi kuzaa matunda mabaya, wala mti mwovu kuzaa matunda mazuri. 19 Kila mti usiozaa tunda zuri hukatwa ukatupwa motoni. 20 Ndiposa kwa matunda yao mtawatambua. 1 Yohana 4: 1 Wapenzi, msiiamini kila roho, bali zijaribuni hizo roho, kwamba zimetokana na Mungu; kwa sababu manabii wa uongo wengi wametokea duniani. SIKILIZA SAUTI 👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾👇🏾